Friday, 20 June 2008

Rostam Aziz na Vodacom-Tususie Ufisadi

Rostam Aziz yule mtanzania mwenye asili ya Kiiran aliyeko kwenye Orodha ya Mafisadi(List of Shame) anamiliki zaidi ya asilimia 30 ya hisa za Kampuni ya Simu za Mkononi ya Vodacom kupitia kwa Kampuni yake ya Caspian ambayo pia inahusika na ufisadi katika kandarasi mbalimbali za ujenzi wa barabara, viwanja na hata migodoni. Je, wewe ni mtanzania unayechukia ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka?

Andika ujumbe huu na mtumie mwenzako mwenye Vodacom kwa SMS:

“Imegundulika, mtaji wa Vodacom sehemu kubwa ni fedha za ufisadi toka kwa Rostam Aziz. Tumia mtandao mwingine kuepuka kulipa fedha zako kuendeleza ufisadi. Ukijitoa kwenye ufisadi, unawapunguzia nguvu mafisadi. Sambaza Ujumbe”Au tuma ujumbe huu:“Afrika Kusini walivunja nguvu ya makuburu. Acha kuendelea kutunisha faida ya Fisadi Rostam Aziz. Achana na kampuni yake ya Vodacom. Tumia mtandao mwingine”.Au:“Je, wajua? Rostam Aziz anahisa nyingi Vodacom kwa fedha za ufisadi. Je, unataka kumwongezea fedha zaidi za kufanya ufisadi nchini? Okoa Taifa, jiunge na simu nyingine”.Au:“Kwanini utende dhambi kwa kuchangia katika ufisadi? Rostam Aziz ni mmoja wa wamiliki wa Vodacom. Tafakari, Chukua hatua”Au:“Ukipiga simu ana kutuma ujumbe kwa kutumia Vodacom unawaneemesha wamiliki mafisadi wakina Rostam Aziz, Noni na makuburu wa Afrika Kusini. Chagua ni lako”Au:“Vodacom, muondoe Rostam Aziz kabla watanzania hatujaucha mtandao wenu kwa kumilikiwa na watuhumiwa wa ufisadi. Tuma ujumbe huu kwenda 123, na mtumie na mwenzio”Au“Ama piga simu huduma kwa wateja namba 100; waulize Vodacom, je Rostam Aziz ni mmoja wa wamiliki? Wanasubiri nini mkutoa kwa ufisadi wake?
Habari za uhakikia kabisa ni kwamba Rostam Aziz ameanza kuhamishia mali zake nje ya nchi, sababu anahofia mambo yanavyokwenda serikalini kwa sasa. Kwa ushahidi tayari ameweka rehani hisa zake zote 35pc za Vodacom Afrika Kusini. Kabla ya kuhamishia hisa zake, alikua amenunua hisa za Planetel za mwenzake Peter Noni na mkewe, naye alifanya hivyo kuhofia mambo yanavyokwenda ofisini kwake BoT. Rostam alichukua hisa zote 35pc za Watanzania kupitia kampuni zake za Caspian na Mirambo. Chenge akiwa Waziri wa miundombinu alimsaidia kwa nguvu zake zote Rostam kufanikisha mkakati wake huo wa kuhamisha hisa zake nje kwa kisingizio cha kuweka rehani. Kuna watu serikalini walipinga (na wanaendelea kupinga) lakini jamaa aliwazidi kete kwa kusadiwa na Chenge na sasa inaelekea amefanikiwa kwa kiasi.

Sheria ya TCRA inasema kuhusu hisa za wazalendo kwamba wageni wasimiliki hisa zaidi ya 65% lakini Rostam Aziz aka RA anataka kuzipeleka nje zote. Inadaiwa kwamba wanatoa kisingizio cha UFISADI alioufanya Mkapa kwa kuuza kinyemela hisa za serikali katika Mobitel (sasa TIGO) na hivyo Tigo sasa inamilikiwa kwa asilimia 100 na wageni lakini sheria inakataza. Wanajaribu kutoa tafsiri ya kisheria kupotosha kwamba eti sheria ilikua na maana na kuanzishwa tu then baadaye mzalendo anaweza kuuza popote wakitoa mfano wa TIGO walkati TIGO ni UFISADI wa Mkapa na genge lake. Sasa Chenge (akiwa Miundombinu) aliandika waraka kwa AG Mwanyika akitoa maeleekezo ya kutaka RA aachiwe auze hisa zake. AG inasemekana alikataa kabla ya kubanwa na kulegeza kamba, na baaaye Bodi ya TCRA ikagawanyika kabla ya kupitisha lakini Management hadi sasa ina maoni tofauti kuhusu uamuzi wa bodi, Inasema sawa, bodi ina uamuzi lakini si kukiuka sheria, sasa kazi ipo maana wanaandaa mabadiliko ya Sheria Ndogo (regulation) ambayo zamani ilikua Waziri anaweza kubadili tu kwa kutangaza katika gazeti la serikali (GN) lakini sasa Samuel Sitta, anaelezwa kuwa kizingiti kwa kuunda kamati ya bunge ya Sheria Ndogo ambayo sasa italazmika kupitia kwanza sheria ndogo kabla haijatangazwa katika GN. Ndio maana kulikua na mkakati maalumu wa kumng'oa Sitta ili kuruhusu hiyo regulation tena inabadilishwa kwa sababu ya mtu mmoja tu, RA.

Hima mtanzania, tuwahawi mafisadi kabla hawajatuwahi. Sambaza ujumbe huu kwenye email za watanzania wengine mpaka kieleweke! Kwa maelezo zaidi wasiliana nami kupitia ashabdala@yahoo.com ama ashawazenj@gmail.com ama tembelea http://ashawazenj.blogspot.com

Kwa nguvu ya umma, tutawashinda mafisadi na kupata Tanzania yenye neema.

Asha Abdala

Monday, 9 June 2008

Suluhisho la Zanzibar

na Mwandishi Wetu
WAKATI harakati za kuyafufua mazungumzo ya kusaka suluhu ya mpasuko wa kisiasa visiwani Zanzibar zikionekana kushindwa, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimesema kina dawa ya kudumu ya mpasuko huo.
Akizungumza na Tanzania Daima mwishoni mwa wiki, Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, alisema mfumo wa majimbo, ambao umeasisiwa na chama hicho, unaweza kuwa suluhu ya matatizo ya kisiasa yanayoikabili Zanzibar hivi sasa.
Mbowe alisema kuwa kitu kikubwa kinachoumiza vichwa kuhusu masuala ya Zanzibar, ni mfumo unaofaa kwa utawala, kutokana na hali halisi kuonyesha kutoshana nguvu kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Wananchi (CUF).
Alisema CUF imeshaonyesha dhahiri kuwa imekikamata Kisiwa cha Pemba, na kwamba hakuna linaloweza kufanyika hivi sasa kidemokrasia kuzuia nguvu za chama hicho kisiwani humo.
“Kinachotakiwa ni kuwaachia CUF waunde serikali yao huko Pemba na chini ya sera yetu ya majimbo jambo hili linawezekana… tunacholenga katika sera hii ni kuwapa watu uwezo na haki ya kujitawala wenyewe, kuamua aina ya viongozi wanaowataka na kujipangia masuala yao wenyewe bila kuingiliwa na serikali kuu,” alisema.
Mbowe alibainisha kuwa, iwapo hilo litafanyika kwa kuanzisha Jimbo la Pemba, CUF wanaweza kuendesha serikali ya jimbo hilo, kama ambavyo vyama vingine vinaweza kuendesha serikali za majimbo watakakoshinda.
Akifafanua, Mbowe alisema kuwa ingawa wapo baadhi ya watu wanaiona sera hiyo kuwa inaweza kusababisha mgawanyiko, lakini iwapo itafuatwa kwa mujibu wa kanuni na taratibu, itasaidia zaidi kuwaunganisha Watanzania.
“Mfumo huu utawapa haki na uhuru zaidi watu wa kujipangia mambo yao, hivyo utawafanya wajione huru zaidi,” alisema na kubainisha kuwa katika mazingira kama hayo, manung’uniko yanayoweza kusababisha chuki miongoni mwa wananchi, yatapungua.
Alisema kuwa dhima kuu ya sera hiyo imegawanyika katika sehemu kadhaa, ikiwamo kurekebisha mfumo wa utawala na kuwawezesha wananchi wa eneo husika kuwachagua viongozi wao wenyewe moja kwa moja.
Alisema mfumo wa sasa ambao baadhi ya viongozi wanateuliwa kama vile wakuu wa mikoa na wilaya, unawafanya washindwe kuwatumikia watu ipasavyo, kwani uwajibikaji wao huwa katika mamlaka iliyowateua na si watu wanaowaongoza.
“Ndio maana tuna wakuu wa mikoa ambao wananchi wengi katika mikoa wanayoiongoza hawawafahamu… wanateuliwa kwa utashi wa mtu mmoja tu na hii ni hatari. Tunachotaka sisi kupitia sera hii ni watu kuchagua viongozi wao katika jimbo lao kutokana na jinsi ambavyo wanawafahamu,” alisema.
Pia, alisema sera hiyo inatasaidia kusisimua uchumi, kwani inalenga kuyafanya maeneo tofauti yashindane kiuchumi.
Mbowe, alisema kila jimbo litakuwa na wajibu wa kukusanya mapato yake, na kuyapangia bajeti ya matumizi, huku likiwajibika kutoa mchango wake kwa Serikali Kuu, kutokana na uwezo wake wa kukusanya mapato.
Alisema Serikali Kuu itaachiwa majukumu manne makubwa na aliyataja kuwa ni uhamiaji, masuala ya ulinzi na usalama, mambo ya nje na masuala ya sarafu na sera za fedha.
“Mtindo wa sasa wa kukusanya mapato yote na kuyaweka kwenye kapu moja (hazina) ni mbaya kwa sababu unawafanya watu wanaodhibiti hiyo hazina wajione kuwa wana fedha, nyingi hivyo kuzitumia hovyo,” alisema.

Sera ya Majimbo Suluhu ya Kisiasa Zanzibar?

CHADEMA: Tuna dawa ya mpasuko Zanzibar